12 Quotes by Enock Maregesi about Secret

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.

  • Tags
  • Share




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Unaweza kuwa umeomba kuhusu jambo fulani kwa muda mrefu bila majibu, lakini siku moja ghafla ukajibiwa wakati umejisahau. Kwa nini? Kwa sababu Mungu hufanya kazi zake kwa siri. Ukiomba jambo kutoka kwa Mungu, huku ukiwa huna kinyongo na mtu yeyote na bila moyo wako kusita wakati ukiomba, tambua katika moyo wako kwamba tayari umeshajibiwa. Kisha lipotezee, hilo jambo, kila siku, usiwe unalikumbukakumbuka, hadi Mungu mwenyewe atakapokujibu. Hata Yesu atakaporudi kila mtu atakuwa amejisahau.

  • Tags
  • Share




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Anayesema fulani ni mwanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru ana hakika? Haya mambo ni siri. Amejuaje? Kumbuka, usiamini, jua!

  • Tags
  • Share