9 Quotes by Enock Maregesi about amani

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kama George Bush angekuwa na amani ndani ya moyo wake na Saddam Hussein angekuwa na amani ndani ya moyo wake Vita ya Ghuba isingetokea. Vilevile, katika kitabu cha ‘Kolonia Santita’, kama Rais wa Tume ya Dunia angekuwa na amani ndani ya moyo wake na kiongozi wa Kolonia Santita angekuwa na amani ndani ya moyo wake Kolonia Santita isingepigana na Umoja wa Mataifa. Taifa lisingepigana na taifa, na mataifa yasingepigana na magaidi.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Nabii wa kweli lazima awe na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi. Kuonyesha usungura wa manabii wa injili ya woga ni jukumu la kila Mkristo wa kweli, kuokoa roho za watu wengi kwa kadiri tutakavyoweza.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.

  • Tags
  • Share