7 Quotes by Enock Maregesi about blood

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Lengo kuu la Kolonia Santita kuuza madawa hayo ni kuwafadhili askari wa msituni wa Kolombia (magorila wa vyama visivyokuwa rasmi vya kisiasa au vyama haramu vya kisiasa) kushika hatamu za uongozi wa Kolombia, kwa makubaliano ya Kolonia Santita kutawala biashara ya kokeini ya taifa hilo la Amerika ya Kusini. WODEA lazima ilizuie Shirika la Madawa ya Kulevya la Kolonia Santita kuuza madawa hayo kwa gharama yoyote ile, pesa au damu, kutetea afya na amani ya dunia.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Siku ya kwanza dhambi ya kwanza ilipotendwa Mungu alitoa kafara ya kwanza ya wanyama kwa ajili ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walikuwa uchi, baada ya kutenda dhambi, Mungu akawalaani lakini akawapa uwezo wa muda mfupi wa kutubu dhambi zao ili awasamehe! Kutokana na ngozi za wanyama hao walipata mavazi na kutokana na damu ya wanyama hao walipata fursa ya kuishi na kutubu dhambi zote walizozitenda. Bila hivyo wasingepata muda wa kusamehewa.

  • Tags
  • Share



  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Damu na maji vilitoka katika mbavu za Yesu Kristo kutokana na upungufu wa damu mwilini, hipovolimia, kulikotokana na kuchapwa bakora. Yesu alichapwa bakora arobaini kabla ya kupelekwa Golgotha. Matokeo ya hipovolimia katika mwili wa mtu ni moyo kwenda mbio kusukuma damu iliyopungua, kuzimia kutokana na msukumo wa damu kuwa chini, figo kushindwa kufanya kazi na kiu ya maji.

  • Tags
  • Share