4 Quotes by Enock Maregesi about lucifer


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Shetani anaweza kukudanganya kwa kukuambia ombeni bila kukoma, wewe ukakesha kuomba na kesho ukaendesha gari lako kuelekea kazini ambako una kikao cha muhimu hali kadhalika. Ukifika kazini unasinzia kwenye kikao unaonekana teja, kumbe ni kazi ya Ibilisi. Tujifunze namna ya kuzipima roho, si kila roho inatoka kwa Mungu.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Wenye dhambi watafufuliwa na wataungana na Ibilisi kuipiga Yerusalemu Mpya itakayokuwa inang'inia hewani, huku Yesu na watakatifu wote wakiwa hawana silaha yoyote; lakini vilevile wakiwa hawapigwi kwa silaha yoyote.Shetani atakapoonekana kushindwa, Yesu atawasha ‘kibiriti cha kiroho’. Mafuta yote yaliyopo ardhini dunia nzima yatalipuka na kugeuza ardhi yote kuwa ziwa la moto, na hivyo wenye dhambi wote kupata aibu ya milele.

  • Tags
  • Share