11 Quotes by Enock Maregesi about right


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.

  • Tags
  • Share




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita hutengenezwa ndani ya mioyo ya watu. Ukiitafuta amani ndani ya moyo wako, taifa halitasimama kupigana na taifa, amani itaweza kupatikana.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Haki hushindana na sheria unapokuwa umeshtakiwa. Kama huna hatia lakini sheria ikasema una hatia, sheria imeishinda haki. Kama una hatia lakini sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria imeishinda haki. Kama huna hatia na sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria na haki vimelingana. Lakini kama utakata rufaa ikathibitika kwamba huna hatia, haki imeishinda sheria.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Fidel Castro alitenda haki katika taifa lake ndiyo maana Mungu akamsaidia yeye na wananchi wake. Ijapokuwa ameondoka, lakini fikira zake sahihi zitaendelea kuwepo. Taifa la Kuba Mungu ataendelea kulibariki, kwa sababu fikira za Wakuba ni fikira za Fidel Castro.

  • Tags
  • Share