111 Quotes by Enock Maregesi about Life






  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Katika Biblia kuna tabiri 333 kuhusu maisha ya Yesu Kristo, na kuhusu kurudi kwake kwa mara ya pili. Kati ya hizo, 332 zilitimia! Bado mmoja tu: Kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili.Unadhani huo wa kurudi kwa Yesu Kristo kwa mara ya pili hautatimia? Muda umefika. Jitathmini katika maisha yako na uchague lililo jema.

  • Tags
  • Share