922 Quotes by Enock Maregesi

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Katika dunia hii tunatakiwa kumwabudu Mungu peke yake. Si mtu au kitu kingine, chochote kile.

  • Share




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Mtu anaweza kusema ana wachumba sita ambao anafikiria kuchagua mmoja kuwa mke au mume. Akichagua kiholela atakuwa na hakika 9% ya kumpata mwenza bora wa maisha. Lakini akitumia ‘optimal stopping’ atakuwa na hakika 37%!

  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kama umeamua kuoa au kuolewa ukiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 40, kulingana na kanuni ya kuachana na ukapera (‘optimal stopping’) umri wa kuwa na msimamo kuhusiana na mtu utakayeoa au kuolewa naye ni baada tu ya kufikisha umri wa miaka 26. Kabla ya hapo kuna uwezekano ukakosa wachumba bora, baada ya hapo wachumba bora wanaweza kuanza kupotea, hivyo kukupunguzia uwezekano wa kumpata mke au mume aliye mwema.

  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Umri sahihi wa kuoa au kuolewa kulingana na kanuni ya ndoa iitwayo ‘optimal stopping’ ni miaka 26. Kanuni hii ya hesabu hujulikana kama kanuni ya asilimia 37, welekeo wa 0.37 wa kumpata mwenza bora zaidi katika maisha yako kuliko wengine wote.

  • Share