922 Quotes by Enock Maregesi




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Bara la Afrika ni tajiri kwa rasilimali kuliko mabara yote duniani. Lakini ni maskini kuliko mabara yote. Cha muhimu si kuwa na rasilimali ardhini. Cha muhimu ni kuwa na rasilimali sokoni.

  • Tags
  • Share




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    A.K.A kirefu chake ni 'Also Known As'. K.K.K kirefu chake ni 'Kadhalika Kikijulikana Kama'. K.N.K kirefu chake ni 'Kadhalika Nikijulikana Kama'. K.A.K kirefu chake ni 'Kadhalika Akijulikana Kama'. Kadhalika, unaweza kusema P.K.K (Pia Kikijulikana Kama), P.N.K (Pia Nikijulikana Kama) au P.A.K (Pia Akijulikana Kama).Tujifunze kuupenda utamaduni wetu, ili vizazi vijavyo visisumbuke.

  • Tags
  • Share