922 Quotes by Enock Maregesi

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kiingereza kililetwa na wakoloni wa Kiingereza kutoka Uingereza na walikitumia katika masuala yote ya kiutawala ya Afrika Mashariki. Kililetwa pia na wamisionari waliojenga shule na kuwafundisha Kiingereza wanafunzi na walimu na watu wengine wa kawaida, kwa lengo la kuwasaidia katika kazi yao ya kueneza dini kama wakalimani, hivyo kufanya Kiingereza kienee zaidi kuliko Kiswahili.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Hata wamisionari, hasa wamisionari wa Kiprotestanti, hawakukitumia Kiingereza katika kueneza dini kwa sababu hadhira yao isingewaelewa. Badala yake walitumia lugha za makabila ya Kiswahili, hivyo kujikuta wakieneza zaidi utamaduni wa Kiswahili kuliko wa Kiingereza au Kijerumani.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Mzazi wako akikwambia kuwa usiwe mkorofi, usivunje sheria za nchi, usiwe na marafiki wabaya, na usiasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukubali. Akikwambia kuwa uwe mkorofi, uvunje sheria za nchi, uwe na marafiki wabaya, na uasi dhidi ya serikali, mheshimu kwa kukataa.

  • Tags
  • Share






  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa sababu wana uwezo wa kuona tusipoweza kuona. Yaani, wanajua kilichokuwepo kabla ya sisi kuzaliwa na wanajua kilichokuwepo baada ya sisi kuzaliwa. Maisha tuliyopitia, wazazi wetu walishapitia. Tulipokuwa, wazazi wetu walishakuwepo; na tulichofanya, wazazi wetu walishafanya. Hivyo, hatuna budi kuwaheshimu wazazi wetu. Lakini, wazazi wetu wanapaswa kujiheshimu kutufundisha adabu na maadili mema.

  • Tags
  • Share