922 Quotes by Enock Maregesi




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu chochote. Wanaweza kuona tusipoweza kuona – nyuma na mbele ya tarehe zetu za kuzaliwa.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Migogoro inatokea kwa sababu watu wameshindwa kuheshimiana. Ukijiheshimu na ukaheshimu wengine; utaacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta, wakati ukiingia.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Haki hushindana na sheria unapokuwa umeshtakiwa. Kama huna hatia lakini sheria ikasema una hatia, sheria imeishinda haki. Kama una hatia lakini sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria imeishinda haki. Kama huna hatia na sheria ikathibitisha kwamba huna hatia, sheria na haki vimelingana. Lakini kama utakata rufaa ikathibitika kwamba huna hatia, haki imeishinda sheria.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kufanya kazi huku ukijua au hujui unavunja sheria ni uhuni. Sheria haina cha kujua au kutokujua sheria.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Shetani anaweza kukudanganya kwa kukuambia ombeni bila kukoma, wewe ukakesha kuomba na kesho ukaendesha gari lako kuelekea kazini ambako una kikao cha muhimu hali kadhalika. Ukifika kazini unasinzia kwenye kikao unaonekana teja, kumbe ni kazi ya Ibilisi. Tujifunze namna ya kuzipima roho, si kila roho inatoka kwa Mungu.

  • Tags
  • Share