922 Quotes by Enock Maregesi
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kiungo chochote kikikuuma ghafla na kuacha au kikiendelea kukuuma kwa muda fulani halafu kikaacha, halafu huna sababu ya kwa nini kinakuuma, angalia unawaza nini wakati kiungo hicho kinakuuma. Kisha lifanyie kazi wazo hilo kwa maombi hata ya sekunde tano! Funika tatizo hilo, hata kama hulijui, kwa damu ya Yesu!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mtu hapa duniani ni jirani yako. Hakuna mtu mwingine hapa ulimwenguni isipokuwa sisi. Lazima tujifunze kuishi pamoja.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Jambo kubwa unaloweza kuwafanyia wenzako ni mfano.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kabla hujaanza … pangilia mawazo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama huijui historia ya Zanzibar kwa nini unajiita Mtanzania? Uzalendo ni pamoja na kuijua nchi yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Usijidharau.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nimebadili utaratibu wangu siku hizi kutokana na maadili ya watoto wetu. Siongei na watoto wangu kuhusu Mungu. Naongea na Mungu kuhusu watoto wangu. Yesu alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Tumrudie; hususan katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hakuna mahali popote katika Agano Jipya ambapo sheria ya Sabato imekomeshwa (Kutoka 31:12-17), kwani Mungu alianzisha Sabato kwa ajili ya wanadamu wote (Marko 2:27). Kinyume cha hapo, Yesu aliitunza (Luka 4:16), Paulo aliitunza (Matendo 17:2) na Wamataifa waliitunza pia (Matendo 13:42-44; 16:13)! Mwandishi wa Waebrania anaandika bila kificho, “Basi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu” (Waebrania 4:9).
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Neno la Kristo ndilo litakalotufanya tuongoke na ndilo litakalotutoa duniani. Tunapokwenda kinyume chake tunaanza kuweka matabaka miongoni mwetu sisi wenyewe.
- Tags
- Share