84 Quotes by Enock Maregesi about People
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maana halisi ya ukarimu si kutoa vitu au mali nyingi kwa watu wanaohitaji msaada, bali ni kutoa vitu au mali hizo bila kinyongo au unafiki wowote. Ukarimu unapaswa kutolewa kwa watu sahihi, wakati sahihi, kiasi sahihi na kwa moyo mmoja bila kinyongo chochote. Ukitoa kwa lengo la kupata faida, huo ni ubinafsi na unafiki mkubwa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
I have written all the 406 pages of my book in Swahili words. Even the countries are in Swahili. Instead of 'Nigeria', for example, I have written 'Nijeria'. That is how it is written in the Swahili dictionary. This can seem as a minor detail and that people may find my mission close to ridiculous! However, single letters and commas matter.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kitabu cha KOLONIA SANTITA kinaweza kusomwa na watu wenye umri wa kuanzia miaka 13 na kuendelea. Katika umri wa miaka 13 fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali. Watoto katika umri huu wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia, na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na uhakika, kama nadharia ya KOLONIA SANTITA.
- Tags
- Share