33 Quotes by Enock Maregesi about Poor
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiwa na elimu huna sababu ya kuwa maskini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera.
- Tags
- Share