13 Quotes by Enock Maregesi about Wealth
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Utajiri wa nje huwa unaanzia ndani, nao ni hekima.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wengi hawana maarifa kwa sababu ya elimu na utajiri. Hawana elimu na hawana utajiri. Nchi iwape wananchi wake kila kitu isipokuwa ujinga na umaskini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Siri kubwa ya utajiri kuliko zote duniani ni mawazo yako.
- Tags
- Share