8 Quotes by Enock Maregesi about adam
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho – Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu – Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kulingana na muda wa Mungu, maisha ya Adamu yalikuwa siku 0.93 au saa 22:32! Maisha ya mwanadamu ni siku 0.07 au saa 1:68!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Adamu ndiye mtu wa kwanza kumjua Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama miaka 1000 ya duniani ni sawa na siku moja ya Mungu; hivyo basi, miaka 930 aliyoishi Adamu ni sawa na siku 0.93 au saa 22:32 za Mungu. Kwa hiyo, ili siku ya Mungu itimie Adamu alipaswa kuishi miaka 70 (siku 0.07 au saa 1:68) zaidi! Ukiidadavua saa 1:68 unapata saa 2:08. Kulingana na muda wa mbinguni tunapaswa kuishi kwa muda wa saa 2:08! Muda huo ni mfupi sana.
- Tags
- Share