5 Quotes by Enock Maregesi about christ
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna watoto wa Mungu na kuna watoto watakatifu wa Mungu. Watoto wa Mungu ni wale waliobatizwa na kumkaribisha Kristo kama kiongozi wa maisha yao, na hata wale ambao hawajabatizwa na kumkaribisha Yesu kama kiongozi wa maisha yao kwa maana ya uumbaji, wakati watoto watakatifu wa Mungu ni mitume na manabii wa kweli.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho – Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu – Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nabii wa uongo atampinga Shetani kwa nguvu zake zote, atakuwa na tamaa ya wanawake au wanaume kama ilivyokuwa kwa Sodoma na Gomora na miji yote iliyoizunguka miji hiyo, na atayadharau mamlaka ya Kristo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mafundisho mengine ambayo si ya kweli ya Ukristo ambayo hutokana na utambuzi wao wa matukio haya ni ‘Siku ya Bwana’. Makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti kote duniani yanaonekana kuwa na nia njema lakini huwadanganya watu kuamini kuwa Kristo alibadili siku ya kupumzika kutoka Sabato kwenda Jumapili. Angewezaje kufanya hivyo? Angeweza kufanya hivyo kwa ufufuo wake!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani.
- Tags
- Share