6 Quotes by Enock Maregesi about harm
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kula sana kunaweza kusababisha virutubisho kuzidi mwilini zaidi ya kiwango kinachohitajika na mwili, ambavyo baadaye vinaweza kusababisha madhara ya papo kwa hapo kama tumbo kuuma au tumbo kujaa gesi! Baada ya muda mrefu wingi wa virutubisho hivi unaweza kuingiliana na ufyonzaji wa madini kama fosforasi, kalisi, magnesi, chuma, na zinki, hali inayoweza kusababisha upungufu mkubwa wa virutubisho, unaoweza kusababisha kifo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Waweza kusema kitu ukadhani umepatia kumbe umeharibu. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuwa mwangalifu unapoongea na watu. Huwajui!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Neno moja kutoka mdomoni mwako linaweza kukuletea madhara makubwa. Fikiria kwanza maana ya kitu unachofikiria (ambacho tayari umekisema kichwani mwako) kabla ya kukisema tena mdomoni mwako. Wenye hekima huzungumza kwa sababu wana kitu cha kuzungumza. Wapumbavu hubwabwaja.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Fikiria kwanza maana ya unachosema. Halafu sema.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kadiri unavyozidi kupanda juu ndivyo utakavyoanguka vibaya.
- Tags
- Share