19 Quotes by Enock Maregesi about heart

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kama George Bush angekuwa na amani ndani ya moyo wake na Saddam Hussein angekuwa na amani ndani ya moyo wake Vita ya Ghuba isingetokea. Vilevile, katika kitabu cha ‘Kolonia Santita’, kama Rais wa Tume ya Dunia angekuwa na amani ndani ya moyo wake na kiongozi wa Kolonia Santita angekuwa na amani ndani ya moyo wake Kolonia Santita isingepigana na Umoja wa Mataifa. Taifa lisingepigana na taifa, na mataifa yasingepigana na magaidi.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Unaweza kuwa umeomba kuhusu jambo fulani kwa muda mrefu bila majibu, lakini siku moja ghafla ukajibiwa wakati umejisahau. Kwa nini? Kwa sababu Mungu hufanya kazi zake kwa siri. Ukiomba jambo kutoka kwa Mungu, huku ukiwa huna kinyongo na mtu yeyote na bila moyo wako kusita wakati ukiomba, tambua katika moyo wako kwamba tayari umeshajibiwa. Kisha lipotezee, hilo jambo, kila siku, usiwe unalikumbukakumbuka, hadi Mungu mwenyewe atakapokujibu. Hata Yesu atakaporudi kila mtu atakuwa amejisahau.

  • Tags
  • Share