9 Quotes by Enock Maregesi about language
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote; au 'pushing the envelope' kwa lugha ya kigeni.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Usipomlea mtoto wako vizuri, atakapopata shida akiwa mkubwa, na wewe utapata shida pia. Kama unadhani ameshindikana, ongea lugha anayoielewa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hata wamisionari, hasa wamisionari wa Kiprotestanti, hawakukitumia Kiingereza katika kueneza dini kwa sababu hadhira yao isingewaelewa. Badala yake walitumia lugha za makabila ya Kiswahili, hivyo kujikuta wakieneza zaidi utamaduni wa Kiswahili kuliko wa Kiingereza au Kijerumani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Lakini Kiswahili kilizaliwa Afrika Mashariki. Kwa nini hatuithamini lugha yetu? Kwa nini hatuzithamini lugha zetu za makabila? Kwa nini hatuipendi na kuitetea lugha yetu ya taifa ambayo ndiyo lugha ya biashara na mawasiliano ya Afrika Mashariki? Kwa nini hatuvitetei vizazi vijavyo kwa kuvitetea vizazi vya leo?
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wajerumani, hata hivyo, wakati wa utawala wao waliruhusu Kiswahili kiwe lugha halisi ya taifa nchini Tanzania kwa vile hawakukiongea Kiingereza wala hawakukipenda. Ndiyo maana Kiswahili kinazungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya au Uganda.
- Tags
- Share