8 Quotes by Enock Maregesi about leo




  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Usimdharau mtu aliyesaidia kukusukuma juu katika ngazi ya mafanikio yako, ikiwa utafanikiwa, kwa sababu kuna leo na kesho. Ukishuka, kama ulimdharau, hatakuamini tena. Lakini ukishuka, kama ulimheshimu, na kama bado ana uwezo wa kukupandisha juu, atakupandisha tena.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Leo ni siku ya kumbukumbu ya giza lililoingia katika familia ya Enock Maregesi. Tarehe 4/11/14 ni siku nuru ya mwanga wa maisha ya nyanya yangu mpenzi Bi Martha Maregesi ilipozimika huko Musoma. Leo ni miaka miwili ametimiza akiwa kimya kabisa! Sikisikii tena kicheko chake wala siisikii tena hekima yake! Familia yake inamkumbuka sana. Palipokuwa kwake ni nyumbani kwetu. Hatuwezi kusahau upendo wake na umuhimu wake kwetu. Tulimpenda sana, lakini Mungu wa mbinguni alimpenda zaidi.

  • Tags
  • Share