25 Quotes by Enock Maregesi about mafanikio
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukifuata kanuni ya nguvu ya uvutano uhitaji kujua jinsi utakavyofanikiwa. Kazi yako ni kuwaza tu kwa namna inavyotakiwa. Waza na amini kwa asilimia mia moja. Mengine yote mwachie Mungu au ulimwengu. Mungu pekee ndiye anayekupa njia na bahati, ili wewe ufanikiwe. Atakupa nguvu ya kufanya kazi na ujanja wowote utakaohitajika, katika harakati hizo za mafanikio yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza. Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna mafanikio ya aina mbili hapa duniani: Mafanikio ya Shetani na mafanikio ya Mungu. Mafanikio ya Shetani ni rahisi kupata na ni ya kitumwa. Mafanikio ya Mungu ni magumu kupata lakini ni ya hakika. Mungu akikubariki, pesa inaongezeka kama inavyoongezeka saa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Siri ya mafanikio ni shida!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha yangu ni kafara ya mafanikio yangu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama huna mama, kama mama yako alishafariki, au kama yupo lakini hakujali, hata kama baba yako yupo au hayupo, mafanikio yako yatatokana na juhudi zako mwenyewe.
- Tags
- Share