6 Quotes by Enock Maregesi about parents
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Biblia inatuagiza tuwaheshimu wazazi wetu ili siku zetu zipate kuwa nyingi hapa duniani. Mzazi wako akikutuma kuiba mheshimu kwa kukataa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu hakutuumba ili tuwe roboti, ambayo hufanya kazi kama ilivyoelekezwa. Alituumba ili tuwe huru. Yaani, tuwe na uwezo wa kuchagua mema au mabaya – ndiyo maana akaweka Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya katika Bustani ya Edeni – ndiyo maana akamtuma Shetani kuwajaribu Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Asiyefundishwa na wazazi wake atafundishwa na dunia kwa kudharaulika.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Isipite siku hata moja katika maisha yako bila kusema hata kimoyomoyo kwa wazazi wako na kwa watu wote wanaokupenda kwamba unawapenda, kwani siku moja hawatakuwepo tena.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wanahitaji elimu na ajira kuwaepusha na janga la madawa ya kulevya.
- Tags
- Share