69 Quotes by Enock Maregesi about shetani


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Jina la Yesu ni kubwa kuliko majina yote duniani na hata kuzimu. Lazima Shetani aliogope kuliko anavyomwogopa Bikira Maria au sakramenti za aina zote. Kumbuka, jina la Yesu halitajwi kilingeni. Linatajwa kanisani, ambapo linatajwa kinafiki. Hivyo, aliye na mamlaka ya kuaminiwa na kuabudiwa na aponyaye ni Yesu Kristo peke yake.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Yesu alikuwa binadamu ili afe kama binadamu kwa ajili ya binadamu. Alikufa msalabani ili sisi wote tuokoke. Lakini Shetani hataki hilo litokee. Akiingilia uumbaji wa Mungu toka tumboni mwa binadamu, binadamu atakayezaliwa hatakuwa na uwezo wa kuongoka. Atakuwa na roho ya jini itakayomjua Shetani badala ya kumjua Mungu. Hivyo kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili hakutakuwa na maana, kwa sababu hakutakuwepo na mtu wa kuokolewa.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Shetani hawezi kujua unafikiria nini: 1 Wafalme 8:39. Yesu anajua unafikiria nini: Yohana 2:25. Shetani haweza kufanya jambo bila ruhusa ya Mungu: Mathayo 4:1. Shetani hawezi kukulazimisha kutenda dhambi: Yakobo 4:7. Pigana na mwindaji wa roho hadi roho yako ikombolewe.

  • Tags
  • Share