18 Quotes by Enock Maregesi about woman
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwanamke mwenye umri wa miaka arobaini na mbili na kuendelea anafaa kuolewa kama ni mjane na ataweza kuwapenda watoto wako kama mama yao alishafariki. Yule ambaye hajawahi kuolewa au aliyewahi kuolewa lakini akaachika bado ni kubahatisha, kwa sababu hujui kwa nini hajaolewa au kwa nini aliachika, hata kama ana watoto.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwanamume kutokana na asili yake atampenda mwanamke hata kama hataonyesha hisia zake kwake. Ukiwaweka pamoja, mwanamume na mwanamke, mwanamume hatafikiri sawasawa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nusu dakika baada ya kuondoa gari, Murphy aliona kiwiliwili cha mtu kikimwendea mbio kutokea katika nyumba ya magaidi! Hapohapo alisimamisha gari na kuacha taa zikiwaka, halafu akashika bunduki na kushuka – akiwa ameangalia mbele kwa tahadhari kubwa. Alikuwa mwanamke. Debbie! Murphy alipojua ni Debbie, alitupa bunduki na kuchomoka mbio mpaka wakakutana na kukumbatiana kwa nguvu! Murphy alimbeba Debbie na kumbusu kila sehemu, halafu akamfuta machozi na kumbembeleza.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.
- Tags
- Share