13 Quotes by Enock Maregesi about Tanzania

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kuna tetesi kuwa Julius Nyerere alipewa tuzo ya MBE na malkia wa Uingereza akiwa rais wa Tanzania! Lakini aliikataa! Kwa nini? Kwa sababu angeonekana Mwingereza zaidi kuliko Mtanzania! Januari 26, 1996 akapewa Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Mahatma Gandhi ya mwaka 1995, ya kwanza kabisa, iliyotolewa na Serikali ya India. Lakini hiyo pia akaikataa! Kwa sababu Mahatma Gandhi alimwaga damu katika harakati zake za kuwang'oa wakoloni barani Afrika! Kama ni kweli, hakuna kujitolea kuliko huko.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Wajerumani, hata hivyo, wakati wa utawala wao waliruhusu Kiswahili kiwe lugha halisi ya taifa nchini Tanzania kwa vile hawakukiongea Kiingereza wala hawakukipenda. Ndiyo maana Kiswahili kinazungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya au Uganda.

  • Tags
  • Share