28 Quotes by Enock Maregesi about Person
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwendawazimu anaweza kuzungumza jambo la maana, kwa maana ya kuongozwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, usimdharau mtu. Kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mtu anapaswa kuwa na siri angalau moja katika maisha yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ningependa – maisha yangu yatakapokoma hapa duniani – kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Si rahisi kumkamata mtu anayeandamana moyoni mwake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kumsahau mtu au kitu usimchukie au usikichukie kwa sababu kuchukia kuna nguvu sawa na kupenda.
- Tags
- Share