30 Quotes by Enock Maregesi about Problems
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Abra maana yake ni fursa. Kwa hiyo, geuza matatizo yako kuwa fursa. Lakini, utageuzaje matatizo yako kuwa fursa? Kugeuza matatizo yako kuwa fursa, amini kama unaweza, usitumie muda mwingi kufikiria tatizo, tumia muda mwingi kufikiria fursa. Ukipata tatizo usikate tamaa. Badala yake, geuza tatizo hilo kuwa faida.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake yote. Fanya kile ulichosema utafanya, hata kama sehemu ya kile ulichosema utafanya uliinukuu kutoka kwa wengine, hata kama watu hawatakubaliana na wewe.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu ni mkubwa kuliko jumla ya matatizo yote na vitu vyote alivyoviumba na ana uwezo wa kufanya kila kitu alichosema atafanya bila kupunguza au kuongeza chochote. Usidanganywe na matatizo. Amka, kabla kifo hakijakufika.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Geuza matatizo yako kuwa changamoto, kuwa abra.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika – kuingia na kutoka kwa hii pumzi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kipo kitu kinaendelea kufanyika katika siku zetu za furaha na katika siku zetu za huzuni kwa kila mmojawetu hapa duniani bila ya upendeleo wowote. Kitu hicho ni kuingia na kutoka kwa pumzi, au kupumua. Ukiithamini pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mwili wako utapata zawadi ya amani katika maisha yako. Utapata pia zawadi ya furaha, uelewa na ufasaha! Ijapokuwa una matatizo mengi katika maisha, kitu bora cha kufanya ni kushukuru Mungu kwa maana wewe ni mzima.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha yangu ni darasa. Jifunzeni kutokana na maisha yangu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za ushupavu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za udhaifu, kutatua matatizo katika maisha yenu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa.
- Tags
- Share