17 Quotes by Enock Maregesi about Universe
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Chumvi si dawa ya kuzuia wachawi au dawa ya kuzuia nguvu kutoka ulimwenguni. Chumvi inazuia wachawi, lakini vilevile inazuia bahati. Dawa halisi ya kuzuia wachawi ni Mwenyezi Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia – Mfumo wa Jua wa Sol – Solar Interstellar Neighborhood – Njiamaziwa – Local Galactic Group – Virgo Supecluster – Local Supercluster – Ulimwengu unaoonekana – Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kabbalah' ni sayansi ya Mti wa Uzima wa Milele wa Bustani ya Edeni au 'The Tree of Life of the Garden of Eden' katika mbingu ya nne, ambayo ni ramani ya ulimwengu na roho ya mwanadamu; au Sayansi ya Mungu, uchawi wa kujua 99% ya siri ya uumbaji wa Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mimi na wewe na vitu vyote ulimwenguni ni wazito kwa sababu ya 'Higgs Boson', inayojulikana pia kama 'The God’s Particle'. Wanasayansi wa CERN wamekuwa wakiitafuta 'higgs' (iliyojificha ndani ya 'higgs field') kwa zaidi ya miaka hamsini sasa, kwa bajeti ya pauni za Uingereza bilioni sita. Chembe ya 'higgs' ikipatikana itawajulisha wanasayansi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi ulivyoumbwa, na jibu la kitendawili cha 'Standard Model' litapatikana.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni.
- Tags
- Share