111 Quotes by Enock Maregesi about life
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Yesu aliishi maisha yake yote chini ya utawala wa kidikteta lakini hakuandamana. Kwa nini sisi leo?
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Yesu wakati anakufa msalabani hakufikiria kifo. Alifikiria maisha.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho – Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu – Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Siri ya utajiri ni mawazo ya mtu. Maisha unayoishi uliyataka mwenyewe. Amka uishi. Hii ndiyo siri kubwa ya utajiri kuliko zote ulimwenguni. Ukifikiria chanya maisha yako yatakuwa chanya, ukifikiria hasi maisha yako yatakuwa hasi. Unachofikiria ndicho unachokuwa. Siri ya mafanikio yako ni jumla ya mambo unayoyawaza.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwonyeshe. Ukionyesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionyesha hasi Shetani atakupa hasi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Usimdharau mtu aliyesaidia kukupa kazi ulipokuwa huna kazi, wala usimdharau mtu aliyesaidia kukulea ulipokuwa mdogo, au mtu aliyeokoa maisha yako au mtu aliyekusaidia kwa namna yoyote ile. Ukimdharau, utakaposhuka, atakusaidia kwa rehema za Mwenyezi Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha.
- Tags
- Share