13 Quotes by Enock Maregesi about wealth
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Utajiri una changamoto nyingi. Yesu alisema ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Hakusema msomi. Usiwe mwendanguu. Jikusuru kuujua ukweli.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza – zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.
- Tags
- Share