134 Quotes by Enock Maregesi about Mungu
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kulingana na muda wa Mungu, maisha ya Adamu yalikuwa siku 0.93 au saa 22:32! Maisha ya mwanadamu ni siku 0.07 au saa 1:68!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Siku ya kwanza dhambi ya kwanza ilipotendwa Mungu alitoa kafara ya kwanza ya wanyama kwa ajili ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walikuwa uchi, baada ya kutenda dhambi, Mungu akawalaani lakini akawapa uwezo wa muda mfupi wa kutubu dhambi zao ili awasamehe! Kutokana na ngozi za wanyama hao walipata mavazi na kutokana na damu ya wanyama hao walipata fursa ya kuishi na kutubu dhambi zote walizozitenda. Bila hivyo wasingepata muda wa kusamehewa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia hii ina watu ambao Mungu anataka kuwaokoa, lakini inafanya wawe wagumu kwelikweli.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wote ni wa Mungu, watu ni matatizo. Wewe huna mtu, lakini bado unapambana na Mungu kuhusu watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kinachosababisha tupambane na Mungu ni matatizo, ambayo huletwa na watu, na tunapambana kwa silaha ya uongo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu haamui jinsi watu wanavyoamua. Mtu akikwambia huna kipaji muulize yeye ni nani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kiongozi kwa sababu ya haki akibarikiwa na Mungu, hata watu anaowaongoza watabarikiwa na Mungu pia. Lakini kama kiongozi amelaaniwa na Mungu kwa sababu ya uovu, hata watu anaowaongoza watalaaniwa pia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie. Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo; watakatifu wasingekuwepo, dunia isingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa. Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.
- Tags
- Share