76 Quotes About Maisha
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kuishi usiogope kufa. Kwa maneno mengine, ukitaka kufanikiwa katika maisha yako, usiogope kufa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kujiponya kisaikolojia lazima unyanyuke kiroho hadi katika ulimwengu wa roho, na uyatazame maisha yako kutokea juu kuja chini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu hutumia majaribu makubwa katika maisha yetu kutukomaza na kutukamilisha. Kitu kisichokuua hukufanya mpiganaji.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Tunapaswa kujisikia furaha kuu tunapokumbana na majaribu mbalimbali katika maisha yetu, tukijua kwamba kujaribiwa kwa imani yetu hutufanya wavumilivu na wapiganaji katika Jina la Yesu, na tunapaswa kuruhusu uvumilivu katika maisha yetu kwa sababu Mungu hutumia uvumilivu huo kutukomaza na kutukamilisha.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.
- Tags
- Share