43 Quotes About Mtu
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anayejaribu kupambana na Mungu anajaribu kupambana na jambo lisilowezekana. Hatakuwa na uwezo wa kushinda. Kufanya hivyo ni upumbavu usioweza kuelezeka, lakini wanadamu hatukomi kufanya hivyo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwendawazimu anaweza kuzungumza jambo la maana, kwa maana ya kuongozwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, usimdharau mtu. Kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mtu anapaswa kuwa na siri angalau moja katika maisha yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hakuna daktari anayeweza kuponya saikolojia ya mtu. Saikolojia ya mtu huponywa na mtu mwenyewe; nje ya ufahamu wa kawaida.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
- Tags
- Share
- Author DON SANTO
-
Quote
Sijafika. Ndio maana simdharau MTU wala hassle yake. Na nitakapofika, bado nitakumbuka Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kupeana riziki.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu humwambia mtu kitu cha kusema na mtu huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Lakini utajuaje kama Mungu amekuchagua wewe kusema au kufanya kitu? Mungu atakwambia kupitia Roho Mtakatifu, na utajisikia msukumo mkubwa wa kusema au kufanya kile ambacho Mungu anataka useme au ufanye. Unabii unaweza kumtokea mtu yoyote, mahali popote, anayejua jinsi ya kuwasiliana na Mungu.
- Tags
- Share