60 Quotes About Watu
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuishi na watu vizuri ni ufundi mkubwa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ubinadamu una kila kitu isipokuwa upendo miongoni mwa watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wenye ujuzi au vipaji wanatakiwa kwenda shule kusomea ujuzi au vipaji vyao – kwa miezi mitatu au sita angalau.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Unataka kufanikiwa lakini hutaki watu wakuone. Kama una kipaji kionyeshe kwa watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia ni mbaya kwa sababu sisi wenyewe ni wabaya. Vitu ambavyo ni viovu ndivyo tunavyovipenda zaidi kuliko vinavyotustahili.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia hii ina watu ambao Mungu anataka kuwaokoa, lakini inafanya wawe wagumu kwelikweli.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna tofauti kati ya haki na utawala wa mabavu. Haki ni jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho. Utawala wa mabavu ni utawala wa kidikteta. Ukitenda haki lazima kuna watu watafaidi. Lazima kuna watu wataumia. Fidel Castro alikuwa kiongozi msahili. Alikuwa kiongozi aliyewezesha kutendeka kwa mambo. Kwa sababu hiyo, wachache walimpenda, wengi walimchukia. Lakini ili ufanye mazuri lazima upambane na mabaya. Shetani mwenyewe hatakuruhusu ufanye mazuri bila kukuletea mabaya.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna watu hawaamini kama Mungu yupo, lakini maisha yao yanaamini.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama umechagua mtu akashinda au akashindwa na matokeo yakatangazwa, idadi kubwa ya watu ikakubaliana na matokeo hayo, umeongea na nchi yako na imekujibu.
- Tags
- Share