60 Quotes About Watu


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Robert Louis Stevenson wa Uskochi aliponukuu nahau ya ‘kamera haiwezi kudanganya’ katika kitabu chake cha ‘South Seas’ mwaka 1896, miaka 57 baada ya sanaa ya upigaji wa picha kugunduliwa, hakumaanisha tuwe asili. Hakumaanisha tusizirekebishe picha zetu baada ya kuzipiga na kuzisafisha! Alimaanisha tuwe nadhifu tuonekanapo mbele za watu au mbele ya vyombo vya habari; ambapo picha itapigwa, itasafishwa, itachapishwa na itauzwa kama ilivyo bila kurekebishwa.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Boresha maisha ya watu kwa kadiri utakavyoweza. Ukisaidia mtu 1 watahurumiwa watu 10. Ukisaidia watu 10 watahurumiwa watu 100. Ukisaidia watu 100 watahurumiwa watu 1000. Kila mmoja wetu akitambua wajibu wake katika jamii, Mungu atatuhurumia sisi wote. Maisha ya mtu mmoja yakiboreka, mmoja huyo ataboresha na ya wengine wengi. Hivyo, endelea kuogelea lakini usisahau kurudi nyuma katika jamii.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Ukitaka watu wakuheshimu usitumie mabavu. Tumia hekima. Maana, watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi, wanaheshimu nguvu ya matendo yako. Kama una tatizo na mtu usichukue uamuzi wa haraka. Ongea na watu kupata hekima.

  • Tags
  • Share