922 Quotes by Enock Maregesi
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi makanisani na misikitini. Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza dhambini huku tunaona, tukiwa mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwendawazimu anaweza kuzungumza jambo la maana, kwa maana ya kuongozwa na Roho Mtakatifu. Hivyo, usimdharau mtu. Kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.
- Tags
- Share