922 Quotes by Enock Maregesi


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kuwepo kwa Mti wa Uzima wa Milele katika Bustani ya Edeni (pamoja) na Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya inamaanisha, Adamu na Hawa walikuwa hai kiroho mpaka walipokula tunda la mti wa katikati ambapo hali yao ya maisha ilibadilika. Adamu na Hawa walikufa lakini hawakufa – walikufa baadaye kabisa. Hii inamaanisha kwamba (haya ni mawazo yangu tu) mtu anapokufa anakuwa amekula tunda la mti wa katikati, litakalomwezesha kuendelea kuishi katika hali nyingine ya maisha ambayo sisi hatuijui.

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Robert Louis Stevenson wa Uskochi aliponukuu nahau ya ‘kamera haiwezi kudanganya’ katika kitabu chake cha ‘South Seas’ mwaka 1896, miaka 57 baada ya sanaa ya upigaji wa picha kugunduliwa, hakumaanisha tuwe asili. Hakumaanisha tusizirekebishe picha zetu baada ya kuzipiga na kuzisafisha! Alimaanisha tuwe nadhifu tuonekanapo mbele za watu au mbele ya vyombo vya habari; ambapo picha itapigwa, itasafishwa, itachapishwa na itauzwa kama ilivyo bila kurekebishwa.

  • Tags
  • Share






  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kama kuna jambo la muhimu unapaswa kufanya kwa ajili ya kadari ya maisha yako na kipindi hichohicho kuna kipindi kizuri cha televisheni unakisubiria, au simu ya umbea, au kinanda cha shida, palilia bustani yako ya kiroho kwa kuachana na televisheni na simu na kufanya jambo la msingi kwa ajili ya maisha yako.

  • Tags
  • Share