922 Quotes by Enock Maregesi


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo lolote na ni tofauti kwa kila mtu. Kama ulivyo uzuri, mafanikio yapo katika macho ya aonaye. Ni jukumu lako kujua mafanikio yana maana gani kwako, na jinsi gani umeyapata mafanikio hayo.

  • Tags
  • Share


  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Kuna siri nyingi za ndani zinazofanya mtu aendelee kufanikiwa, na kuna siri nyingi za nje zinazofanya mtu aendelee kuficha siri ya mafanikio yake. Siri za ndani ni siri za kweli, ilhali siri za nje ni siri za uongo, zenye lengo la kuficha ukweli. Hata hivyo, siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, pamoja na siri.

  • Tags
  • Share



  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Yesu Kristo hakufa siku ya Ijumaa jioni na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi. Alikufa siku ya Jumatano jioni na kukufuka siku ya Jumamosi jioni. Wakati kifo kinamkumba, hakuwa na umri wa miaka 33, alikuwa na umri wa miaka 31. Kama Yesu Kristo alikufa siku ya Ijumaa jioni, na kufufuka siku ya Jumapili asubuhi, hatuna Mwokozi!

  • Tags
  • Share

  • Author Enock Maregesi
  • Quote

    Hii ni muhimu sana kwa Pasaka. Si tu kwamba Pasaka ni tamasha linalojitegemea, lakini kadhalika linatumika kama siku ya maandalizi kwa ajili ya siku takatifu, siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu. Kwa mujibu wa hesabu za kalenda ya Kihebrania, Pasaka inaweza kuangukia siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijumaa au Sabato.

  • Tags
  • Share