12 Quotes by Enock Maregesi about History
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristo waliamua kufa kinyama kulinda heshima ya mfalme wao Yesu Kristo, kama Biblia na historia vinavyosema. Kwa nini watu (wengine) wa kizazi hiki wanasema hakuna Mungu na kwa sababu hiyo hawamwamini Yesu? Je, uko tayari kufa kwa ajili ya mtu aliyekufa kwa ajili yako? Kwa ajili ya mtu ambaye mitume walikuwa tayari kufa kwa ajili yake? Je, wewe una akili zaidi kuliko mitume? Yesu aliamua kufa ili wewe uishi, lakini bado unakuwa mbishi. Badilika.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote; au 'pushing the envelope' kwa lugha ya kigeni.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Israeli na Palestina ulianzishwa na Israeli mwenyewe. Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Vita ni vilevile, ukoloni ni uleule, ubaguzi ni uleule, umaskini ni uleule, harakati za kijamii ni zilezile, matabaka ni yaleyale. Kwa nini tusiseme historia inajirudia? Tunatakiwa kujifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya katika historia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
WWPP ('WODEA Witness Protection Programme') ni Programu Maalumu ya Ushahidi ya Tume ya Dunia ya kuwakinga mashahidi wa kihalifu kwa kuwapa makazi mapya, majina mapya, kazi mpya, historia mpya ya maisha, na sura mpya, kuwakinga na Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ukivunja Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika cha Kolonia Santita utauwawa, tena utauwawa kinyama, wewe na familia yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.
- Tags
- Share