10 Quotes by Enock Maregesi about humans
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anayejaribu kupambana na Mungu anajaribu kupambana na jambo lisilowezekana. Hatakuwa na uwezo wa kushinda. Kufanya hivyo ni upumbavu usioweza kuelezeka, lakini wanadamu hatukomi kufanya hivyo.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani hawezi kusoma ndani ya myoyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Usimpe nafasi Shetani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Damu ya Mwanakondoo ina nguvu kuliko maombi. Mungu hauwi, Anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Ukifunikwa na damu ya Mwanakondoo Shetani, ambaye ni wakala, hatakuona. Lakini Mungu atakuona. Bila kafara ya damu hakuna msamaha wa dhambi. Bila kafara ya damu hakuna mafanikio.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani anapenda damu kumtumia Mungu kwa faida yake kama vile Mungu anavyomtumia Shetani kwa faida yake. Mungu anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu, na Shetani anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu. Mungu anaishi ndani ya damu na damu ina nguvu kuliko Shetani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani naye anamtumia Mungu kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu kwa sababu Shetani siku hizi anaishi makanisani na misikitini. Anamtumia Mungu kwa maana ya kutuingiza dhambini huku tunaona, tukiwa mbele ya uwepo wa Mungu tunayemwabudu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.
- Tags
- Share