7 Quotes by Enock Maregesi about nature
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu alimuumba mwanadamu ili aitawale dunia. Shetani tayari alikuwepo wakati Adamu anaumbwa. Adamu na Hawa walipokula tunda la mti wa katikati, walikufa kiroho – Yaani, walipoteza sura na asili ya Mungu – Shetani akawashinda kuanzia kipindi hicho na kuendelea. Tulizaliwa katika dhambi. Kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Njia pekee ya kuikomboa sura na asili ya Mungu ni kumpokea Yesu (Kristo) kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua. Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nimeishi na watu kutoka katika mabara yote ya dunia hii. Wanaume wana asili yao na wanawake wana asili yao. Ndiyo maana katika upendo wa PHILADELPHIA, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri, wanaume na wanawake hawachangamani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwanamume kutokana na asili yake atampenda mwanamke hata kama hataonyesha hisia zake kwake. Ukiwaweka pamoja, mwanamume na mwanamke, mwanamume hatafikiri sawasawa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwanamume hataweza kumwelewa mwanamke na mwanamke hataweza kumwelewa mwanamume. Kwa sababu asili zetu ni tofauti.
- Tags
- Share