15 Quotes by Enock Maregesi about Talents
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Fanya kazi kwa bidii na maarifa!
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu anapokupa kipaji anategemea ukitumie vizuri kwa ajili ya wengine. Usipokitumia vizuri kwa ajili ya wengine, ama kwa uvivu au kwa woga, atawapa wengine wakitumia kwa ajili yako. Ukitumia vipaji vyako vizuri, Mungu atakuongezea maradufu. Yaani, ukitumia muda wako vizuri atakuongezea muda. Ukitumia nguvu zako vizuri atakuongea nguvu. Ukitumia pesa yako vizuri atakuongezea pesa. Ukitumia ukarimu wako vizuri atakuongezea ukarimu. Ukitumia maarifa yako vizuri atakuongezea maarifa.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukitaka kujua vipaji vyako ulivyopewa na Mungu mtumikie Mungu katika kitu fulani kwa nguvu zako zote.
- Tags
- Share