24 Quotes by Enock Maregesi about Wisdom
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwenye hekima huzungumza kilicho na maana! Kinaweza kuwa kizuri au kibaya.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea Roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea Roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hekima ni ufunguo wa kufanya maamuzi mema kulingana na msingi wa maarifa ya Biblia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu anaweza kuchanganyikiwa lakini akasema kitu cha hekima, akiongozwa na Roho Mtakatifu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Simama nyuma ya maneno uliyoyasema mara mbili: kichwani na mdomoni mwako. Simama nyuma ya maneno uliyoyasema kwa hekima. Usiyumbe hata mambo yatakapokwenda segemnege.
- Tags
- Share