111 Quotes by Enock Maregesi about life
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiua mtu bila kumwambia kwa nini unamuua anaweza kujua umemuua kwa kumwonea. Akijua umemuua kwa kumwonea roho yake inaweza kukusumbua wewe na familia yako maisha yenu yote. Makachero wa EAC wana leseni ya kuua. Lakini si kuua ovyo kama James Bond. Kila wanayemuua lazima waandike ripoti kwa nini wamemuua. Kachero wa EAC akiua mtu, kwa makosa, kwa bahati mbaya, atalindwa na Mwenyezi Mungu. Atalindwa na Tambiko la Tume ya Dunia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuna vita za aina mbili zinazopiganwa hapa duniani: vita ya maisha na vita ya dhambi. Unaweza kushinda vita ya maisha (maisha ya raha) lakini ukashindwa vita ya dhambi (maisha ya laana). Kushinda vita ya dhambi ni lazima umkaribishe Mwana wa Mungu Mfalme wa Amani, Yesu Kristo wa Nazareti Aliye Hai, kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Vita ya dhambi hupiganwa katika uwanja wa akili na katika uwanja wa mwili kati ya Shetani na Mungu. Hutumia silaha kuu ya uongo na silaha kuu ya ukweli. Mungu anataka tuujue ukweli. Shetani anataka tuujue uongo. Kushinda vita ya dhambi huna budi kutumia neno la Mungu, kama Yesu alivyolitumia kumshinda Shetani wakati akijaribiwa katika Mlima wa Majaribu wa Jangwa la Yuda.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani. Ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nini kingetokea kama Adamu na Hawa wasingekula tunda la Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya mpaka siku ya Sabato? Mungu angewaruhusu kula na lengo la uumbaji wa Mungu lingekamilika. Wanadamu wakifuata Amri Kumi za Mungu katika maisha yao watakuwa na uwezo maalumu ambao baadaye utawawezesha, kupitia Roho Mtakatifu, kuwa na maarifa ya siri ya uumbaji wa Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli?
- Tags
- Share