111 Quotes by Enock Maregesi about life
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kama mwanadamu una haki ya msingi kuwa na amani katika maisha.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ningependa – maisha yangu yatakapokoma hapa duniani – kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Live as you were created to live.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa sababu wana uwezo wa kuona tusipoweza kuona. Yaani, wanajua kilichokuwepo kabla ya sisi kuzaliwa na wanajua kilichokuwepo baada ya sisi kuzaliwa. Maisha tuliyopitia, wazazi wetu walishapitia. Tulipokuwa, wazazi wetu walishakuwepo; na tulichofanya, wazazi wetu walishafanya. Hivyo, hatuna budi kuwaheshimu wazazi wetu. Lakini, wazazi wetu wanapaswa kujiheshimu kutufundisha adabu na maadili mema.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika – kuingia na kutoka kwa hii pumzi.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kipo kitu kinaendelea kufanyika katika siku zetu za furaha na katika siku zetu za huzuni kwa kila mmojawetu hapa duniani bila ya upendeleo wowote. Kitu hicho ni kuingia na kutoka kwa pumzi, au kupumua. Ukiithamini pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mwili wako utapata zawadi ya amani katika maisha yako. Utapata pia zawadi ya furaha, uelewa na ufasaha! Ijapokuwa una matatizo mengi katika maisha, kitu bora cha kufanya ni kushukuru Mungu kwa maana wewe ni mzima.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Maisha yangu ni darasa. Jifunzeni kutokana na maisha yangu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za ushupavu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za udhaifu, kutatua matatizo katika maisha yenu.
- Tags
- Share