98 Quotes About Dunia
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia hii ina watu ambao Mungu anataka kuwaokoa, lakini inafanya wawe wagumu kwelikweli.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Watoto hawatakiwi kuchungwa kupita kiasi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. Uhuru utakaowanyima wakiwa wadogo watakuja kuutafuta baadaye wakiwa wakubwa. Wakiutafuta baadaye wakiwa wakubwa hawataeleweka vizuri katika jamii. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata lakini si uhuru wa kila kitu.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie. Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo; watakatifu wasingekuwepo, dunia isingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa. Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Dunia nzima imejaa giza! Kupenya lazima uwe jasiri.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nimeishi na watu kutoka katika mabara yote ya dunia hii. Wanaume wana asili yao na wanawake wana asili yao. Ndiyo maana katika upendo wa PHILADELPHIA, upendo wa wanachama wa mashirika ya siri, wanaume na wanawake hawachangamani.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mungu anatupenda sana, ndiyo maana akamleta Mwanawe wa pekee ili afe kwa ajili yetu, lakini haupendi mfumo wa maisha wa dunia hii.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Yesu Kristo wa Nazarethi ni mtu mashuhuri zaidi kuliko wote kuwahi kukanyaga ardhi ya dunia hii. Alikufa majira ya saa 9 kamili za mchana, siku ya Jumatano, katika kipindi cha demani cha AD 31. Saa chache baadaye, jua lilipokuwa likizama, alilazwa katika kaburi jipya la Yusufu wa Arimathaya. Katika siku ya kawaida ya Sabato, Jumamosi, siku tatu kamili baada ya mazishi yake, Mungu Baba alimfufua Mtoto Wake kwa ajili ya uzima wa milele.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mbegu zilizopandwa kwenye udongo wenye rutuba ni rahisi sana kuvamiwa na magugu iwapo mwenye bustani hataipalilia bustani yake kila siku. Kila siku tunapaswa kupalilia bustani zetu za kiroho, kuondoa magugu ambayo ni raha za dunia hii.
- Tags
- Share