18 Quotes by Enock Maregesi about Family
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa na sehemu ya upendo wa AGAPE. Alijitahidi kuwapenda wengine kuliko yeye na familia yake.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ofisi si rafiki wa familia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Ukiua mtu bila kumwambia kwa nini unamuua anaweza kujua umemuua kwa kumwonea. Akijua umemuua kwa kumwonea roho yake inaweza kukusumbua wewe na familia yako maisha yenu yote. Makachero wa EAC wana leseni ya kuua. Lakini si kuua ovyo kama James Bond. Kila wanayemuua lazima waandike ripoti kwa nini wamemuua. Kachero wa EAC akiua mtu, kwa makosa, kwa bahati mbaya, atalindwa na Mwenyezi Mungu. Atalindwa na Tambiko la Tume ya Dunia.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwanampotevu dunia ilimfundisha ndiyo maana akarudi kwa baba yake akiwa amenyooka, hakuwa na maadili mema. Yusufu dunia ilimfundisha ndiyo maana akawa waziri mkuu wa Misri, na ndiyo maana akaokoa familia yake kutokana na njaa, alikuwa na maadili mema. Heri kudharaulika kwa kutenda mema kuliko kudharaulika kwa kutenda maovu. Ukidharaulika kwa kutenda maovu hutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukidharaulika kwa kutenda mema Mungu atakuinua.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.
- Tags
- Share
- Author Enock Maregesi
-
Quote
Mandela alikuwa hodari ndiyo maana akapelekwa jela. Alikuwa mvumilivu ndiyo maana akakaa jela kwa miaka ishirini na saba. Alivyotoka akawa kiongozi bora wa Afrika Kusini. Utu ukafanya awasamehe binadamu wenzake. Urithi wa Nelson Mandela kwetu ni uhodari, uvumilivu, uongozi bora, utu na msamaha kwa binadamu wenzetu. Mandela alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Afrika Kusini alikuwa mlezi wa ndoto, ya amani na uhuru.
- Tags
- Share