#Mtu

Active
43quotes
Explore
Standalone tag

Quotes about mtu

"
Lolote unalolifikiria yupo mtu mahali fulani duniani ameshalifikiria.
"
Mtu anaweza kuchanganyikiwa lakini akasema kitu cha hekima, akiongozwa na Roho Mtakatifu.
"
Utamsaidiaje mtu aliyekukosea? Msamehe!
"
Endeleza nafsi yako katika kujitegemea, kwani ukishaifundisha nafsi yako kujitegemea hutamtegemea mtu.
"
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu.
"
Mtu akikupa pesa kwa ajili ya kufanyia kitu kibaya chukua. Kisha ipeleke polisi, ambapo utatoa taarifa zake pia.
"
Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa? Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.
"
Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda.
"
Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.
"
Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma.
Showing 1 to 10 of 43 results